Saturday, 9 June 2018

Naibu waziri Nishati aridhishwa na ubora wa Luku za wawekezaji wa ndani

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwa ameshika moja ya mita za Luku za kisasa (Smart Meter), inayotengenezwa na kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania kilichoko Mbezi, Dar es Salaam, wakati alipotembelea kujionea mita hizo jana Juni 8, 2018.Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, akizunguza jambo baada ya kujionea mita hizo.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akimsikiliza meneja mwandamizi wa Tanesco anayeshuhghulikia Mauzo na Masoko, Mhandisi Theodory Bayona.

Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto) akiangalia utaalamu wa kutengeneza mita hizo.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa pili kushoto) akiangalia utaalamu wa kutengeneza mita hizo.

Moja ya mita hizo ikiwa katika hatua za mwisho za matengenezo.

Wataalamu wa kiwanda ambao wote ni Watanzania wakiwa kazini.

Subira Mgalu, akitoa maelekezo kwa meneja mwandamizi wa Tanesco anayeshughulikia mauzo na masoko wa Tanesco, Mhandisi Theodory Bayona.

Mwenyekiti wa Bodi ya Kiwanda cha Baobab Engineering System Tanzania, Allan Magoma, akizungumza wakati wa ziara hiyo ya naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.


K-VIS BLOG/KhalfanSaid

NAIBU Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametembelea kiwanda cha kutengeneza mita za Luku kilichoko Mbezi jijini Dar es Salaam.

Ziara hiyo ilifanyika jana Juni 8, 2018 ambapo naibu waziri huyo ameridhishwa na ubora wa mita hizo.

Amesema tatizo la mita lilikuwa ni changamoto kubwa iliyopelekea kasi ya kuwafikishia umeme Watanzania kwenda mwendo wa kinyonga baada ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco), kuagiza mita nje ya nchi ambazo hazikuwa zikiingizwa kwa wakati.

Kampuni ya Baobab Engineering System Tanzania ndiyo watengenezaji wa mita hizo za kisasa za  Luku (Smart Meters) na uongozi wa kiwanda umeahidi kuzalisha za kutosha ili kutatua changamoto iliyokuwa ikiikabili Tanesco kuhusu upatikanaji wa mita hizo.

“Sisi katika kutaka shirika letu la Tanesco lifanye vizuri tumewapa maelekezo yako ndani ya Sera na mipango yetu lazima waunganishie umeme wateja wengi na moja ya ‘component’ inayotakiwa ni mita.

Kumekuwa na changamoto ya mita kama mlivyosema, na hasa inatokana na utaratibu wa uagizaji na hata kufika kwa vifaa hivyo ilichukua muda sana, sasa uwepo wa kiwanda cha kutengeneza mita hapa nyumbani ninaamini tatizo hili sasa halitakuwepo,” amesema Mgalu.

Kwa upande wake, Meneja mwandamizi wa Tanesco anayeshuhghulikia mauzo na masoko, Mhandisi Theodory Bayona amesema tayari Shirika limeanza kutekeleza agizo hilo la serikali na mchakato wa ununuzi umeanza kwa kuhakikisha vifaa vyote vya shirika vinanunuliwa kutoka ndani na tayari Tanesco imeanza kununua nguzo za umeme hapa hapa nchini.

Lakini kuhusu mita za umeme Tanesco ina mpango wa kununua mita 350,000 kutoka kwa wawekezaji wa ndani ambazo zitatumika kubadilisha zile mita za zamani ambazo hazikuwa zikienda sawasawa.

Awali  naibu waziri huyo alipatiwa maelezo ya kiuntendaji ya kiwanda hicho kabla ya kupata fursa ya kutembelea eneo la uzalishaji ambapo alijionea namna mafundi wazawa wa kiwanda hicho wanavyotengeneza mita hizo la Luku.

No comments:

Post a Comment