Monday, 11 June 2018

Tanesco Manyara kuwachukulia hatua kali wanaohujumu miundombinu


Maneja wa Tanesco mkoa wa, Manyara Gerson Manase akizungumza na wanahabari hawapo pichani hivi karibuni katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya shirika hilo.

Mwandishi Wetu,

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) mkoa wa Manyara limewatahadharisha wakazi wanaoendelea kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya shirika hilo kuwa wakibainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Tahadhari hiyo imetolewa na meneja wa Tanesco mkoa huo hivi karibuni, Gerson Manase kupitia kampeni maalumu inayofanywa na Tanesco makao makuu ikiwa na lengo la kuhamasisha kuhusu athari za kuhujumu miundombinu ya shirika na kufanya shughuli karibu.
“Kuanzia sasa mkazi yoyote atakaye kiuka sheria na kufanya shughuli za kibinadamu karibu na miundombinu ya umeme, tutafyeka mazao yake yote na hatua nyingine za kisheria zitafuata,” amesema meneja huyo.

Kwa sasa Tanesco Manyara inahudumia wilaya tatu za Babati, Mbulu na Kateshi ambapo kuna wateja wapatao 28,000 na lengo ni kuongeza idadi zaidi.

Mitambo iliyosimikwa ina uwezo wa kuzalisha megawati 50 ila kwa sasa matumizi ni megawati 15 tu na kukaribisha wawekezaji kwani umeme upo wa kutosha.

Amesema wakazi hao walishalipwa fidia zao na shirika ili kupisha maeneo hayo ambayo ni hatarishi kwa maisha yao lakini kuna baadhi bado wanafanya shughuli za kilimo.

Aidha, amesema katika maeneo hayo kuna vyombo vya moto huwa vinatakiwa kupita kwa ajili ya ukaguzi wa miundombinu sasa wakati mwingine inashindikana kutokana na watu kupanda mazao katika njia hizo, matokeo yake kazi zinashindwa kufanyika kwa wakati.

Meneja amesema, “Tunatoa mwito kwa wakazi wote waheshimu sheria kwani tulishaandika barua kwa wenyeviti wa vijiji kuhusiana na azma yetu. Lengo la shirika sio kumkomoa mtu ila na kuhakikisha maisha ya watu yanakuwa salama na umeme unapatikana kwa wakati,”

Katika hatua nyingine meneja huyo aliomba wakazi kuachana na tabia ya kuhujumu miundombinu hiyo na kuongeza mkoa huo umekithiri kwa wizi wa nyaya za umeme.

Alisema wizi huo unarudisha jitihada za shirika nyuma na maendeleo kwa ujumla kwani serikali inatumia gharama kubwa kwa ajili ya marekebisho.

Akitolea mfano hivi karibuni kuna wizi wa transformer ulitokea na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wateja na shirika kwa ujumla, “Vitendo hivi vinaweza kuleta maafa makubwa, badala ya kuhujumu tunaomba washirikiane na sisi kukomesha wizi huu,”

Naye Kaimu Meneja Kitengo cha Mawasiliano Tanesco Leila Muhaji amesisitiza kwamba zoezi la uhamasishaji linafanyika nchi nzima lengo ni kutoa elimu ya madhara yanayoweza kupata watu wanaojaribu kuiba vifaa au kufanya shughuli karibu ya miundombinu ya umeme.

8 comments:

 1. The our de France 2018 will be the 105th edition of the Tour de France, one of cycling's three Grand Tours. The 3,329 km race will depart Noirmoutier-en-l'Île, in the Vendée department, on 7 July and will finish with the Champs-Élysées

  stage in Paris, on 29 July. A total of 176 riders across 22 teams will participate in the 21-stage race. The Tour will be the shortest of the century and will be the fifth time a tour has set out from the Vendée department.

  tour de france 2018
  https://tourdefrance.wiki/
  https://defrancetour.de/
  https://tourfrancede.de/
  https://francedetour.de/
  https://tour-defrance.org/
  https://tourde-francelive.com/
  http://tour-defrance-live.blogspot.com/

  ReplyDelete