Thursday, 7 June 2018

Tango, asali tiba mujarabu ya macho


Tango

MACHO kuwasha, kuuma au kuona kiiza uendako ni matatizo ambayo yanawakumba watu wa rika zote licha ya kuwa wazee wapo hatarini zaidi kukumbwa nayo.

Zipo tiba za asili na kisasa ambazo zimekuwa zikiwasaidia waathirika wa matatizo hayo kuondokana nayo.

Kimsingi naelezea hatua za tiba asili ambazo mgonjwa anaweza kupata nafuu au kupona kabisa.

Kinachotakiwa mgonjwa anayekabiliwa na moja ya matatizo hayo anatakiwa alale chali kisha aweke kipande cha tango katika jicho lake ili majimaji ya tango hilo bichi yaingie ipasavyo jichoni.

Zoezi hili liendelee ndani ya kipindi cha siku 10 ambapo utaona mabadiliko makubwa. Baada ya muda huo paka asali katika jicho (macho) kwa muda wa siku tatu.

Tiba hizi zifanyike jioni kabla ya kwenda kulala. Licha ya kutibu macho, matango husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huhitajika mwilini, hii ni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha maji.


Maji hayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, dawa na vinywaji tunavyovitumia kila siku.
Tunda hili pia husaidia kupunguza uzito wa mwili kwa kuwa lina asili ya nyuzi nyuzi (fibres), humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini ambavyo husababisha aongezeke uzito.
Ulaji wa tango husaidia kupunguza uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi aamke bila uchovu.
Tango pia husaidia katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na ulaji wa matango pia husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.


Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment