Thursday, 7 June 2018

Tumia maua ya m-boga kupunguza uchungu wakati wa uzazi


Maua ya m-boga

MMEA wa boga (m-boga) ni maarufu kaika maeneo mengi hapa nchini. Majani ya m-boga yapo kwenye kundi la mboga za majani.

Matunda yake (maboga) yanatumiwa na makabila mengi hapa nchini kama chakula baada ya kuyapika.

Wakati mmea wa boga tunaufahamu kama chakula, maua yake yana maajabu makubwa katika tiba.

Pamoja na kutibu magonjwa mengine, maua ya boga yanasaidia kupunguza uchungu wakati wa uzazi, yanaondoa maumivu ya tumbo la hedhi na kurekebisha hedhi isiyo na mpangilio.

Pia yanasaidia kuondoa tatizo la kutopevusha mayai kwa wanawake walioko katika umri wa kuzaa, yanaongeza wingi wa maziwa kwa kinamama wanaonyonyesha, yanaongeza mbegu za uzazi kwa kinababa na kuwawezesha kudumu katika tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Namna ya kutumia maua ya maboga kwa tiba, chukua kilo moja yapike kwa muda wa dakika 10 hadi 15 kisha kula kama supu. Tumia kwa muda wa siku mbili asubuhi na jioni.

Zingatia maelekezo ni tiba nzuri kwa tatizo lako la kiafya. Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 pia tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment