Saturday, 9 June 2018

Wajua mti wa fulu unasafisha na kupevusha mayai?


Fulu
YAPO matunda ya kupandwa na ya porini ambayo ni mazuri kutokana na radha yake tamu au baridi. Fulu ni moja ya matunda pori ambayo ni maarufu katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Kwenye baadhi ya mikoa ikiwemo ile ya Kusini matunda hayo yakijulikana kwa jina hilo, mikoa ya kanda ya Ziwa yanajulikana kama sungwi. Mmea (mfulu) unaozaa matunda haya matamu kumbe ni tiba kuanzia matunda hadi mizizi yake.

Mizizi ya fulu inasaidia kusafisha nyumba ya uzazi na kupevusha mayai kwa wanawake wenye tatizo hilo, lakini pia ni tiba kwa wenye vidonda vya tumbo.

Chukua mizizi ya mfulu ichemshe muda wa dakika 15, kisha maji yake weka katika kikombe cha chai kunywa kimoja asubuhi na kingine jioni.

Majani ya mfuru yakichemshwa yanasaidia kuratibu kisukari na shinikizo la damu katika kiwango cha kawaida kisicho na madhara.

Juisi ya fulu inasaidia kwa wanaosumbuliwa na tatizo la vidonda vya tumbo, ambapo mwenye tatizo hilo atengeneze juisi ya matunda haya na kuitumia mara nyingi awezavyo.

Kutokana na tunda hili kuhesheni kiwango kikubwa cha protini na vitamini A, B na D husaidia pia kuimarisha mifupa.

Kwa kawaida hapa nchini matunda haya yapo ya aina mbili, yale yenye rangi nyeusi na mengine kijani.

Mada hii imeletwa kwako kwa ufupi nami mtaalam wa tiba, lishe na virutubisho, Abdalallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya, karibu makao yetu makuu Ukonga Mongo la ndege, Dar es Salaam au wasiliana nami kwa simu namba 0745900600 pia tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com ili kuelimika zaidi na masuala ya kiafya.

No comments:

Post a Comment