Saturday, 9 June 2018

Zantel yasitisha mauzo ya laini za simu kupitia mawakala


KAMPUNI ya Simu za mkononi Zantel imesimamisha mauzo ya laini zake za simu kwa mawakala wake wakuu kuanzia sasa.

Uamuzi huo umekuja baada kuwepo tuhuma za kuwepo kwa matumizi mabaya ya mtandao huo.

“Zantel imedhamiria kuzingatia na kusimamia sheria zote na kanuni zote pamoja na kufuata viwango vya juu vya maadili na kampuni haitavumilia vitendo vyovyote vya udanganyifu kupitia mtandao wake.

“Tunashirikiana na mamlaka za serikali kushughulikia tuhuma za makosa haya na tutachukua hatua zote ili kuepusha hatari zaidi katika suala hili.

“Zantel inawahakikishia wateja wake kuwa hakuna madhara kwenye huduma zinazotolewa kwao na wateja wanaweza kuendelea kutumia huduma na kununua laini za simu katika maduka ya Zantel na mawakala wake usajili wa laini za Zantel,” imesema taarifa hiyo iliyotolewa na uongozi wa Zanzibar Telecommunications PLC.

No comments:

Post a Comment