Tuesday, 30 April 2019

MAVI YA TEMBO YANAPONYA DEGEDEGE KWA WATOTO


Mapokezi ya mtoto anapozaliwa yakikosa umakini kidogo tu yanaweza kusababisha apate tatizo katika ubongo.

Madhara huanza kuonekana anapofikisha umri wa kuanzia miezi sita.

Mara nyingi umri huo hadi miaka miwili anaweza kupata tatizo la  ugonjwa wa kuanguka hata kama hakuwahi kukumbwa na homa inayochangia tatizo hilo.

Mtoto anapoanguka (degedege), familia nyingi zimekuwa zikikimbilia kumpa mafusho ambayo wakati mwingine siyo mazuri kupewa mtoto  mwenye  umri wa chini ya miaka 10.

Ni vema wanafamilia wanapobaini tatizo hilo kwa mtoto  wao waende kwa madaktari bingwa au baadhi ya matabibu  tiba asili wa magonjwa ya watoto ambao wanaweza kuwasaidia.

Tangu enzi za mababu walitumia kinyesi cha tembo kile alichojisaidia punde kikiwa kingali cha moto kukabiliana na tatizo hilo.

Kinyesi hicho kichanganywe na mafuta ya mbono au ya nazi  au ya nafaka kisha kumchua mwilini mtoto  mwenye  tatizo hilo.

Wakati akifanyiwa tiba  hii apewe chakula chenye virutubisho kilichosheheni oksijeni na glucose ambacho kitakwenda katika ubongo wa mtoto kusaidia kuirudisha mishipa ya damu katika hali ya kawaida.

Chakula hicho kinaweza kuwa ni uji uliotokana na   mchanyiko wa muhogo, ulezi na mbegu za maboga baada ya kusagwa pamoja.

Ikiwa una swali kuhusu jambo lolote unaweza kuwasiliana nami kwa 0745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com.

No comments:

Post a Comment