Thursday, 16 May 2019

LOZI NI KINGA NA LISHE

Mbegu za mlozi (Almond seeds), ambazo ni jamii ya njugu, hazina umaarufu mkubwa miongoni mwa wanajamii walio wengi hapa nchini.

Mbegu hizi ambazo huliwa kwa kutafunwa kama karanga baada ya kuzikaanga kidogo, zina utajiri mkubwa wa protini na virutubisho mbalimbali kama madini ya shaba (copper), ambavyo husaidia kuratibu mfumo mzima wa mwili.

Kula mbegu tano za lozi kila siku zinasaidia kukukinga na maradhi ya saratani ya utumbo na tumbo la uzazi. Ndani ya lozi mna madini yanayosaidia kuimarisha misuli, viungo, mifupa na kukabiliana na shinikizo la damu.

Zipo aina mbili za lozi ambazo ni tamu na chungu.

Lozi tamu ndizo huliwa, nazo pia zipo zenye ngozi nyembamba na nene.

Lozi chungu zina prussic acid ambayo ni sumu, aina hii zinatumika kutengenezea vitu vya urembo kama mafuta na manukato ( purfumes).

Hapa Afrika, Morocco na Afrika Kusini ndizo nchi zinazostawisha kwa wingi milozi ambao asili yake ni Mashariki ya kati.

Faida nyingine ya lozi ni kusaidia kuondoa tatizo la tumbo kuunguruma, vidonda vya tumbo, usanisi wa chakula tumboni kufanyika vizuri na kuongeza wingi na ubora wa mbegu za kiume.

Kwa wenye upungufu wa nguvu za kiume na kike, watafune lozi kwa wingi na wakoma wasage mbegu hizo na kisha wajipake palipo na tatizo.

Hapa nchini maeneo ambayo unaweza kuzipata lozi ni katika masoko makubwa na kwenye supermarket.

Katika mkoa wa Morogoro inaelezwa kuwa zao hilo linastawishwa lakini kwa kiwango kidogo.

Iwapo una swali au tatizo kiafya unahitaji ufafanuzi unaweza kunipigia kwa 0745900600 au kuniandikia kwa barua pepe (e-mail) dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment