Wednesday, 19 June 2019

WAJUA KWIKWI IKIZIDI NI TATIZO? FANYA HAYA UONDOKANE NAYO

      Iriki
      Sukari

Mara nyingi mtu hushikwa na kwikwi baada ya kiwambo cha moyo kupata karaha.

Hali hii hudumu katika kipindi cha kisichozidi dakika 20, inapozidi zaidi ya muda huo au hata siku nzima, linaweza kuwa tatizo linalohitaji ufumbuzi.

Kwikwi inaweza kumpata mtu wa jinsia na rika lolote, huku wajawazito na watoto wachanga wsmekuwa wakikabiliwa na tatizo hilo kwa kiwango kikubwa zaidi.

Wataalamu wa masuala ya afya ya uzazi wanasema wakati wa ujauzito uwezo wa mwanamke kuvuta hewa ndani ya mapafu huongezeka kwa asilimia kati ya 30 hadi 40 ikilinganishwa na pale anapokuwa hana mimba.

Hata hivyo, kwa upande wa watoto hususan wachanga, hakuna sababu ya kitaalamu inayojulikana kuwa ndiyo inasababisha wapate kwikwi, zaidi sana wazazi wanashauriwa kutotishwa na hali hiyo inapowapata watoto hao.

Kundi jingine ambalo wakati mwingine hukumbwa na tatizo hilo ni wale waliofanyiwa upasuaji.

Kama nilivyosema awali kwikwi ni tendo linalozuka ghafla na hudumu muda mfupi, linapochukua muda mrefu unaweza kutumia moja ya njia hizi kukabiliana nalo.

A) KIKONYO CHA NYONYO

Jaza maji baridi ndani ya kikonyo cha nyonyo, kunywa kidogo kidogo muda wa dakika tatu hadi 10.

A) HOFU

Fanya kitu ambacho kinaweza kumshtua au kumwopesha mtu mwenye kwikwi na mara hali hiyo itakoma.

C) MAJI BARIDI

Chukua glasi yenye maji baridi ongeza kijiko kimoja cha asali kisha koroga. Kunywa polepole lakini mfululizo hadi maji yote yaishe.

D) KUZUIA PUMZI

Bana pua na zuia pumzi kwa muda mrefu uwezavyo, wakati huo kunywa pia maji baridi.

E) SUKARI

Shinikiza shingo iende upande wa kushoto na kulia kwa vidole gumba vya mikono kisha lamba kidogo kidogo sukari iliyojaa katika kijiko hadi iishe.

F) IRIKI NA MNANAA

Pondaponda iriki tatu pamoja na majani matano ya mnanaa, chemsha na glasi moja ya maji, baada ya kuipua, acha ipoe hadi hatua ya kuweza kunywewa, kunywa polepole hali ya kwikwi itatoweka. 

Kwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji, asitumie dawa yoyote bila ushauri wa madaktari.

Ikiwa una tatizo lolote la kiafya, karibu katika kituo chetu Ukonga, Mongolandege, Dar es Salaam.

Tunajali mgonjwa wa aina yoyote. Tunahudumia kwa kutumia tiba lishe na virutubisho asilia.

Pia kama una tatizo la kiafya ungependa kuwasiliana nami nipigie kwa 0745900600 au niandikie kwa barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Au tembelea tovuti yetu kwa anuani ya www.dkmandai.com ambapo utajifunza mambo mengi yanayohusu afya yako.

No comments:

Post a Comment